Breaking News

Bonge la Nyau afungukia mahusiano yake na Shilole

Msanii wa bongo fleva Bonge La Nyau amesema hana mahusiano ya kimapenzi na Shilole japo watu wamekuwa wakiwaona karibu kiasi cha kuzusha kwamba wawili hao ni wapenzi.
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Bonge la Nyau amesema kwa sasa yeye ana mpenzi wake ambaye wamejaliwa kupata mtoto mmoja hivyo watu wanaposema yeye na Shilole wapo karibu sana ni kutokana na kuwaona pamoja kwenye picha lakini pia yeye na Shilole wanaendana ndiyo sababu watu wamekuwa wakihisi kwamba ni wapenzi.
Hata hivyo Bonge la Nyau amesema yeye na Shishi ni washkaji sana na popote pale watu watakapo waona wakiwa pamoja waelewe kwamba wao ni marafiki tu lakini hawana mahusiano yeyote ya kimapenzi na kwamba haiwezi kuwa hivyo kamwe.
Mtazame Bonge la Nyau akifunguka kwenye show hii ya eNewz